Wednesday 7 September 2011

Serikali ipunguze matumizi

Report ya wataalam wa IMF wameshauri serikali yetu ibane matumizi ili iweze kuimarisha uchumi. Uchumi wetu unakua kwa kiwango cha kiridhisha mwaka ulioisha (7%). Kuna sekta, idara na wizara ambazo serikali imeweza kuziboresha sana  (mfano utendaji jeshi polisi, baraza la mitihani etc). Lakini tunatakiwa kupunguza matumizi fulani na kuelekeza pesa zaidi kwenye matumizi mengine ya kimaendeleo zaidi. Kwa mfano, kununua magari ambayo yanatunagharimu sana (kwa manunuzi na uendeshaji) na kununua magari ambayo ni nafuu. Kupunguza posho na kuelekeza pesa hizo kwenye matumizi ya kimaendeleo, n.k.